AyoTV

VIDEO: Kauli ya Waziri Mwigulu kuhusu mauaji ya wenyeviti Kibiti

on

Siku kadhaaa zimepita tangu kutokee mauaji ya Mwenyekiti mstaafu wa CCM wilayani Kibiti Pwani ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake, tukio hilo ni mfululizo wa matukio ya mauaji  mkoani Pwani.

Leo May 21 2017 Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba ametembelea eneo la Kibiti kwa mara nyingine na kuzungumza na askari polisi ambao wako kwenye operesheni ya kuhakikisha wanakomesha matukio hayo, na hiki ndicho alichokisema…..

“Hatutawaacha wanaoua na wala hatutawaacha wanaoshirikiana na wanaoua, hakuna chama cha siasa ambacho kina thamani sawa na uhai wa binadamu, mtu kuwa chama anachotaka hajafanya kosa hata kustahili kuuawa, kwa maana hiyo mimi kila nikitafakari naona kuna kamchezo kanakochezwa”-Waziri Mwigulu

VIDEO: Majibu ya Waziri Nchemba kwa wanaosema amekaa kimya Kuhusu watu kutekwa, Bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments