Mwigizaji Irene Uwoya amefunguka siku ya jana mbele ya waandishi wa Habari kuhusu kampeni yake mpya ya Jembe ni Mama aliyoitambulisha leo na kuzindua mbele ya waandishi wa Habari ikiwa na lengo la kusaidia wanawake kupitia kilimo ambacho kimekua ni kiinua mgongo cha Taifa
Irene amezungumza mbele ya waandishi wa Habari na kusema “Sekta ya kilimo ndio mhimili mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi hapa nchini na Watanzania zaidi ya milioni 40 wanajishughulisha na kilimo na kutegemea kilimo katika lishe na sehemu ya kujikwamua kiuchumi,sasa sisi pamoja na Wizara ya kilimo leo tumeanzisha kampeni mradi inayoitwa ‘JEMBE NI MAMA’
Lengo la mradi huu ni kusaidia wizara ya kilimo kusukuma gurudumu la kilimo bora na chenye maslahi kwa wanawake wote ili kumuwesesha mkulima mwanamke anayefanya kilimo duni katika jamii yake”
Uwoya pia aliongezea kwa kusema “Sisi kamaJembe ni mama tutaanza kutembelea wakulima wote wanawake ndani ya Tanzania ili kutambua changamoto wanazokutana nazo wanawake wanaojishughulisha na kilimo na jinsi gani wanaweza kuelemika kuhusu kilimo cha kisasa na jinsi gani wanaweza kuelimika kuhusu biashara yao kwenye kilimo wakaona faida yao kwa ajili ya familia zao na Taifa kwa ujumla”
Hata hivyo katika mkutano huo kulikuepo na Muheshimiwa Angelina Kairuki, Mama Terry na wadau wengine wakiwemo mama Ongea na Mwanao walioongozwa na Steve Nyerere Pamoja na wanawake waliowahi kufanya kilimo kwa ukubwa