Habari za Mastaa

Mwigizaji kutokea Marekani Harvey Weinstein akutwa na Corona Virus

on

Mwigizaji na Mtayarishaji maarufu wa filamu nchini Marekani Harvey Weinstein ameripotiwa na vyombo vya habari kuwa amekutwa na maambukizi ya virusi vya Ugonjwa wa Corona.

 

 Hapo awali Weinstein alihukumiwa kifungo cha miaka 23 Jela kwa makosa ya ubakaji na unyanyasaji wa Kingono.

Msemaji wa Idara ya magereza mjini New York ameuthibitishia mtandao wa The Daily Beast kwamba kuna wafungwa wawili wamekutwa na maambukizi ya Corona katika gereza la Wande Correctional Facility, japo hawakuanika majina ya wafungwa hao ambao tayari wametengwa.

 

Tupia Comments