Top Stories

Mwigizaji Shilole aolewa… hizi ni picha zake na Rommy

on

Mwigizaji ambae pia ni Msanii wa Bongofleva Shilole amefunga ndoa na Mchumba wake Rommy, Shilole amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram na hii inakuwa ndoa yake ya pili rasmi baada ya ile ya kwanza aliyofunga na Uchebe kuvunjika.


Baada ya kuweka picha hizi za kuthibitisha ndoa Shilole ameandika yafuatayo ——> “Namshukuru Mungu, tumemaliza salama, kwa sasa unaweza kuniita Mrs Rajabu Issa (Rommy)”

Shilole na Rommy walianza uhusiano wao mwanzoni mwa mwaka 2009 baada ya kukutana Tanga na penzi lao lilikaa kwa mwaka mmoja tu kisha wakaachana na kila mtu kuendelea na maisha yake ikiwemo Rommy kuoa na Shilole kuolewa, baadae wawili hawa wakarudiana baada ya ndoa zao kuvunjika na hii ilikuwa ni mwaka 2020.

Mwanzoni wakati waliporudiana wawili hawa walikataa kuthibitisha kama ni kweli mpaka ilipofika December 20, 2020 ndiyo wakakubali kuwa mapenzi yamerudi na hii ilikuwa ni kwenye birthday party ya Shilole ambapo Roomy alimaliza mchezo siku hiyohiyo kwa kumvalisha Shilole pete ya uchumba na leo April 22 2021 wawili hao wamefunga ndoa, Shilole ana Watoto wawili wa kike ambao Rommy amemkuta nao na Rommy ana Mtoto ambaye Shilole amemkuta naye.

ULIPITWA??? BALAA LA SHILOLE NA SHABIKI YAKE JUKWAANI…

Soma na hizi

Tupia Comments