Habari za Mastaa

Mwimbaji Adele uingiza Bilioni 1.6 za kitanzania kwa show moja

on

Mwimbaji mwenye uraia wa Uingereza aishie nchini Marekani, Adele ameripotiwa na vyombo mbalimbali kuwa ulipwa kiasi cha  fedha za kimarekani dola $700,000 kwa show ya siku moja.

Taarifa hizo zimeibuka baada ya kulipwa katika show moja iliyofanyika huko Las Vegas Nevada huko Marekani, Kiasi cha pesa hicho kinakadiriwa ni sawa na Bilioni 1.6 za kitanzania.

Inaelezwa shavu hilo uambatanishwa na chumba atakacholala chenye thamani ya fedha za kimarekani  $ 30,000 ambazo ni sawa na Milioni 70 za kitanzania.

Adele kwasasa anapeta na album yake mpya aliyoingiza Soko mwaka jana inayokwenda kwa jina la 30 Album ambayo bado inaendelea kufanya vizuri.

Tupia Comments