Kampuni ya Str8upvibes imetangaza ujio wa Tamasha la muziki ambalo linatarajiwa kufanyika wikiendi hii Jumamosi tarehe 3 Desemba 2022, ujio wa Tamasha hilo kuwaburudisha wadau wa muziki.
Akizungumza Mkurugenzi mtendaji Str8upvibes Bw. Sniper Mantana amesema lengo la kuwepo kwa burudani hiyo ni kuhakikisha watanzania wanapata kile kilichobora hususani kwenye masuala ya burudani.
“Lengo letu ni kuhakikisha tunaikata kiu ya mashabiki wa muziki kama utakumbuka tumeshaingia kwenye rekodi mbalimbali ya kuwaleta wasanii na ndio utamaduni wetu na wikiendi hii tutakuwa na msanii wa Nigeria Skales ambae atatoa burudani katika viwanja vya Golden Tulip Dar es Salaam, na milango itakuwa wazi kuanzia mchana saa nane nawakaribisha wadau wote wanaopenda muziki mzuri”- Sniper Mantana
Unaweza ukazitazama hapa baadhi ya nyimbo za Mkali Skales ambae atatumbuiza Dar es Salaam Golden Tulip.