Stori Kubwa

Mwanamke wa miaka 46 kapambana na Jambazi na kumpokonya bunduki Tarime..

on

Ni Mwanamke kutoka Mara ndio amechukua headlines wakati huu, anaitwa Sophia Steven na umri wake ni miaka 46, kwa mujibu wa riporter kutoka Mara, Mwanamke huyu alizawadiwa na Jeshi la Polisi kiasi cha Sh. laki 5 baada ya kupambana na majambazi na kufanikiwa kumpokonya mmoja bunduki aina ya SMG.

Sophia anasema hii sio mara yake ya kwanza kuvamiwa na Majambazi, ilishawahi kutokea mwaka 2014 nyumbani kwake na akapambana hivyohivyo na Jambazi mmoja lakini Sophia akazidiwa nguvu baada ya Jambazi huyo kuita wenzake, wakamsaidia na walimjeruhi sana mama huyu.

Polisi wamesema silaha Sophia aliyompokonya Jambazi huyo ni bunduki ya kivita na inatakiwa kumilikiwa na serikali tu, bunduki hii imekutwa na risasi 27, ‘Mama huyu alijitoa kimasomaso kuhakikisha anamdhibiti mtu aliyekua amebeba silaha hii, tunampongeza sana alisema Kamanda Mushi, kamanda wa mkoa wa kipolisi Rorya.

Ukitaka kumsikia Mwanamke mwenyewe akizungumza bonyeza play kwenye hii video hapa chini…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments