Mix

Picha 10: Mbunge Mwita Waitara katolewa nje ya bunge baada ya kutaka kuanzisha vurugu

on

Bunge la 11 limeendelea tena leo Dodoma ambapo Wizara ya Katiba na Sheria ilikuwa ikiwasilisha mpango wa makadirio ya bajeti kwa mwaka 2016/2017 kupitia kwa Waziri wake Harrison Mwakyembe.

Baada ya kuwasilisha kazi ikawa ni zamu ya Wabunge kuchangia bajeti hiyo, lakini hali ikabadilika wakati Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustino Hole alivyopata nafasi ya kuchangia akaanza kwa kutoa kauli kuwa ‘Tundu Lissu ana cheti za Milembe‘ kauli ambayo ilionysha kutowpendeza baadhi ya Wabunge wa kambi ya upinzani.

Ghafla Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara akainuka na kuanza kupiga kelele kuonyesha kutofurahishwa na kauli hiyo kisha kuanza kusimama na kuanza kupiga meza.

Naibu Spika Tulia Ackson Mwansasu akamtaka mbunge huyo kukaa chini, Waitara hakuonyesha kutii amri ndipo Naibu Spika akaamulu askari Polisi wa bunge kumtoa nje ya bunge.

Nimekusogezea hizi 10 za mwanzo, endelea kukaa na millardayo.com kwa taarifa zitakazoendelea kunifikia… 

AW1A0570

Mbunge Augustino Hole akiongea

AW1A0620

Augustino Hole akizuiwa kuzungumza

AW1A0632

Mwita Waitara akiondoka kwenye kiti chake kumfuata Augustino Hole

AW1A0654

AW1A0669

Askari wa Bunge wakimtoa Mwita Waitara

AW1A0679

AW1A0687

AW1A0707

AW1A0740

Nje ya Bunge, Askari wakimsindikiza Mwita Waitara

AW1A0752

.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments