AyoTV

BREAKING: Meya wa Mwanza aliekamatwa na Polisi akimpokea Rais Magufuli, aongea

on

Zilitoka taarifa za Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire kushikiliwa na Polisi uwanja wa ndege Mwanza wakati akisubiria kumpokea Rais Magufuli, leo Meya huyo ameita Waandishi wa habari na kueleza yafuatayo.

“Nilipata mwaliko wa kwenda kumpokea Rais uwanja wa ndege, nikiwa kwenye mabanda ya kuuza chai pale walitokea Askari Polisi wawili na kusema wanataka kuongea na mimi, nikaambatana nao kwenda Polisi na walinishikilia kwa masaa sita”

“Waliniambia nikae pale ndani nipumzike kwa muda mpaka msafara wa Rais uwe umekamilika, wakatokea Askari wengine watatu nusu saa baadae wakaniambia natakiwa kuhamia kituo cha kati, nikawauliza nina kosa gani? wakasema wamepata taarifa kuna kitu kibaya nimekiandaa….. nikawaambia wanithibitishie”

“Wakaniambia ngoja tukwambie ukweli kwamba sisi tumepata maelekezo kutoka juu, kutoka juu tumeelekezwa na RCO kwamba wewe upumzike huku mpaka swala zima la Rais liweze kukamilika ndio baadae tutakuachia” – Bwire

Kufahamu yote aliyoyasema James Bwire mpaka mwisho bonyeza play kwenye hii video hapa chini

VIDEO: Mama alieangua kilio mbele ya Rais Magufuli Mwanza na maagizo ya Rais Magufuli baada ya kumsikiliza, bonyeza play hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments