Michezo

Simba yamfungukia Juuko Murshid “Hatujamlipa na hawezi lazimisha kuondoka”

on

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba Crescentius Magori ametolea ufafanuzi suala la Juuko Murshid ambaye inatajwa ameonesha utovu wa nidhamu ndani ya Klabu hiyo akiwa ndani ya mkataba unaomalizika December mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari  amenukuliwa akisema “Wakati timu imeenda Kanda ya Ziwa, alisema anaumwa (kweli aliumia) akabaki Dar akiuguza majeraha, timu ilivyorudi Dar tayari alikuwa ametoroka ameenda Uganda hakuwepo kwenye kambi ya timu, tukacheza mechi za mwisho akiwa hayupo, hakutoa taarifa kwa Kocha, Meneja wala Uongozi.”

“Baada ya siku chache tukasikia yupo kambini na timu ya Taifa ya Uganda anafanya mazoezi, tukamwandikia barua ajieleze ni kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuondoka kwenye kituo chake cha kazi bila ruhusa ya Mwajiri hata kuongea na Kocha wala Meneja, hiyo barua hakuijibu hadi leo” Magori

“Juzi tumemwandikia barua wakati Simba inaanza kambi tukamwambia aripoti kituo chake cha kazi kabla ya July 15 lakini bado hajaripoti” Magori

“Juuko anafikiri kwamba anaweza kulazimisha kihama, hawezi kulazimisha. Na kwa sababu alitoroka kazini, mshahara wa mwezi wa May na June hatukumlipa, tunamlipaje mtu ambaye hayupo kazini?” Magori

“Kama kuna timu amepata aje hiyo timu ije izungumze na Simba .” Magori

TAZAMA BONGO ZOZO ANAVYOENDA UWANJANI MECHI YA TAIFA STARS NA KENYA

Soma na hizi

Tupia Comments