Michezo

CONFIRMED: Azam FC wamemalizana na John Bocco

on

Siku moja baada ya mitandao ya kijamii kuandika kuwa mshambuliaji wa Azam FC John Bocco amejiunga na Simba, taarifa ambazo bado hazina uhakika wowote, leo May 26 Azam FC wamethibitisha kuachana na John Bocco.

Azam FC leo kupitia kwa afisa habari wake Jafari Idd Maganga wameweka wazi kuwaJohn Raphael Bocco hatoendelea kuitumikia Azam FC kuanzia msimu ujao kutokana na mchezaji huyo kumaliza mkataba wake.

Jafari Idd kupitia SportExtra ya Clouds FM amethibitisha kuwa John Bocco sio mchezaji wao tena hivyo swali au ishu yoyote inayomuhusu John Bocco atafutwe mwenyewe.

Unaweza kutazama mahojiano ya Mkurugenzi wa SportPesa na AyoTV baada ya kuingia mkataba.

Soma na hizi

Tupia Comments