Top Stories

Mzee afia lodge kisa viagra

on

Polisi katika Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya wanachunguza kifo cha Mwanaume moja mwenye umri wa miaka 55 ambaye amefia lodge wakati akifanya mapenzi huku chanzo kikidaiwa kuwa ni kuzidisha kiwango cha dawa za kuongeza nguvu za kiume (viagra) ili aweze kumridhisha kingono Msichana wa miaka 25 ambaye alikuwa nae lodge.

Mwanaume huyo ambaye jina lake limefichwa na Polisi anadaiwa kuanguka ghafla akiwa katikati ya tendo na baadaye kufariki akiwa kwenye Lodge hiyo iliyopo eneo la Ndhiwa.

“Mwanaume huyo alichukua chumba kisha dakika chache baadaye akaja Msichana wa miaka 25 wakajumuika nae chumbani wakiendelea kujivinjari ghafla majanga hayo yakatokea na Msichana akatoa taarifa kwa Uongozi wa Lodge hiyo kuwa Mzee amezidiwa”

“Msichana amekiri mbele ya Polisi kwamba alikuwa anafanya mapenzi na Mzee huyo na kwamba anahisi alitumia viagra ili kuongeza nguvu za kiume na huenda ndizo zimemletea matatizo, Msichana huyo anashikiliwa Polisi kwa uchunguzi zaidi” ——— POLISI KENYA

Soma na hizi

Tupia Comments