Top Stories

Mzee Gerodi ameuawa na Mwanae

on

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamtafuta Jailos Haule, kwa tuhuma za mauaji baada ya kumpiga na kitu chenye ncha kali Baba yake mzazi, Gerodi Haule (72), mkazi wa Mawengi wilayani Ludewa mkoani humo, hali iliyopelekea kusababisha kifo chake.

RPC Njombe Hamis Issah, amesema tukio hilo imesababishwa na uwepo wa ugomvi wa kifamilia na imani za kishirikina, uliopelekea kutoelewana kati ya baba na mtoto, ambapo mara baada ya mzee huyo kujeruhiwa, alipelekwa hospitali na baadaye kufariki baada ya hali yake kuwa mbaya.

“Kuna mzee mmoja ameuwawa ana umri wa miaka 72, kutokana na kuwepo kwa ugomvi wa kifamilia ulioleta hali ya kutoelewana, kutokana na mtoto mmoja kwenye familia hiyo kugombana na baba yake na kuchukua kitu chenye ncha kali na kumjeruhi mzee wao” Kamanda Issah.

LIVE MAGAZETI: Mwisho wa ubishi, JPM kazi nzito kushinda Urais 2020

 

Soma na hizi

Tupia Comments