Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Nuh Mziwanda alivyotaka kuingizwa kwenye biashara ya dawa za kulevya

on

Najua kuna wakati unatamani kufahamu changamoto wanazopitia wasanii wa Bongo Fleva sasa time hii nakusogezea stori ya Nuh Mziwanda ambaye yeye amefunguka na kukiri kukutana na changamoto ya kutaka kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Akiongea na ripota wa millardayo.com alisema…‘Kwanza hii hali ya mimi kuambiwa niuze dawa za kulevya ndio niweze kupata hela ya kusaidia muziki ilikuwa baada ya kuona mambo yalikuwa hayaendi kipindi nikiwa chini ya Dar Stamina’ – Nuh Mziwanda

‘Kwa hiyo baada ya mimi kutoka Dar Stamina nikawa natafuta meneja atakayesimamia kazi zangu basi mara nikapata meneja ambaye alitaka mimi nijihusishe katika biashara ya dawa za kulevya, yeye alitaka niwe nasambaza hapa Dar na aliniambia atakuwa ananilipa laki moja kwa siku kwa hiyo sikukubaliana naye kwasababu sikuwa na ndoto ya kufanya biashara hiyo’ – Nuh Mziwanda

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments