Top Stories

Mzozo eneo la Karume, Serikali ya Zanzibar yatoa kauli (Video+)

on

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema uwepo wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu  Nyerere visiwani Zanzibar  ni kielelezo Chanya katika kuenzi na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa Vitendo.

Makamu wa Pili wa Rais  wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameleza hayo kupitia hotuba alioisoma kwa niaba ya Rais Dk. Hussein Mwinyi  katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi  wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere – Kampasi ya Karume Zanzibar.

‘Suala la mzozo Mkuu wa chuo amelizungumza na mimi nilitaka kumuhakikishia kwamba kwa niaba ya Mheshimiwa Rais hili suala tutalimaliza kwa kipindi kijazo’- Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar

 

Tupia Comments