Habari za Mastaa

U HEARD: Majibu ya Abubakar Mzuri baada ya kudaiwa kufumaniwa na mke wa mtu

on

October 24, 2016 Ndani ya U Heard ya Clouds FM amesikika msanii Abubakari Mzuri ambaye wiki iliyopita kupitia U Heard kulikua na stori yake juu ya kudaiwa kufamaniwa na mke wa mtu. Leo mtangazaji Soudy Brown amempata Aboubakar Mzuri na kuzungumza naye kuhusu taarifa hizo. 

Aboubakar Mzuri amesema kuwa hakuna ukweli wa tukio hilo na kudai kuwa suala hilo limetengenezwa na watu ili kumchafulia tu sifa yake kwa jamii huku akikataa kujibu chochote kuhusu tukio hilo la fumanizi na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la Mjomba.

Hizo ni taarifa zenu ndio zinasema hivo, kwanza namba yangu umeipata wapi? Ulitakiwa kumuuliza QS Mhonda au kunipigia kwanza mimi ujue nini kilitokea sio kukurupuka na kusema vitu ambavyo hamjui vikoje. Mimi ni mtu maarufu mlitakiwa kunitafuta kwanza huenda nilivamiwa na majambazi je?:- Aboubakari Mzuri

ULIPITWA NA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO OCTOBER 24? TAZAMA HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments