AyoTV

VIDEO: Bunge limetaka kujadili kitendo cha aliyemtukana Rais Magufuli kuchangiwa fedha

on

June 21 2016 Mbunge wa Nchemba Juma Nkamia alisimama bungeni kuomba mwongozo wa bunge kujadili tukio la mtuhumiwa wa kesi ya kumtukana Rais Magufuli kuchangiwa fedha na watu kwa ajili kulipa fidia, kitendo kinachoashiria dharau. Mwongozo wa Nkamia ukaungwa mkono pia na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde.

Nkamia alisema…>>>’Kuna mtu alimtukana Rais na akahukumiwa kwenda jela au kulipa faini ya milioni 7, alilipa nusu ya faini ile na akaruhusiwa aondoke akatafute fedha nyingine. Nilitaka wanasheri watusaidie, hivi kumtukana Rais wa nchi alafu yule aliyetukana anaruhusiwa akatafute fedha za kulipa‘ –Juma Nkamia

Siku ya kukabidhiwa fedha anaita na waandishi wa habari, na baadhi ya wabunge humu ndani wa chama fulani walionyesha wananchangia fedha yule mtu ili akalipe faini. Kwahiyo ni maana kuwa alitumwa na chama hicho akamtukane Rais.’ –Juma Nkamia

Sasa naomba kujua sio dharau kwa Rais? sheria inaruhusu jambo hili kufanyika? na kama mimi leo nikahukumiwa kwa kesi ya kuiba kuku siwezi kuruhusiwa kutafuta fedha, iweje mtu huyu akaruhusiwa kutoka nje kutafuta fedha na bado akaonekana watu wakimkabidhi fedha? hizi ni dharau kwa taifa kwa ujumla‘ –Juma Nkamia

Hapa chini nimekusogezea full video…

ULIIKOSA HII? EXCLUSIVE YA WAZIRI NAPE KUHUSU WABUNGE WA UPINZANI WANAOSUSIA BUNGE

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa  INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments