Top Stories

Press ya kwanza ya Paul Makonda baada ya kumalizana na Wahariri

on

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefanya mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa habari August 10 2017 toka alipomalizana na Jukwaa la Wahariri August 16 2017 na kumuondolea kikwazo cha kutotangaza habari zake.

Kwenye Press hii ya kwanza, Paul Makonda amewataka wakazi wa Dar es Salaam wenye ulemavu wa miguu na wanahitaji miguu ya bandia, wafike katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kupimwa na kupewa miguu hiyo katika zoezi litakalofanyika August 14 na 15, 2017.

Ameifanya hii baada ya kutafuta na kupata Wadhamini ambao wamekubali kusaidia miguu ya bandia 200 ambayo itagaiwa kwa watu wenye ulemavu ili kuwasaidia kuweza kufanya shughuli zao kama kawaida ambapo katika awamu ya kwanza itagaiwa miguu 200 huku mguu mmoja ukiwa na thamani ya Tsh. Milioni 3.

Soma na hizi

Tupia Comments