Premier Bet SwahiliFlix Ad Halotel Ad

Habari za Mastaa

Taylor Swift aongoza list ya waimbaji wakike wanaoingiza pesa nyingi

on

Imeripotiwa kuwa jarida la Forbes limetoa list mpya ya majina ya mwaka huu 2019 inayojumuisha wasanii wa kike wanaolipwa pesa nyingi kupitia kazi zao za muziki, list hii imeangalia kuanzia June 2018 mpaka June 2019.

Katika list hiyo mwimbaji Taylor Swift anashika nafasi ya kwanza na kutajwa kuwa anaingiza kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 185 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 400 za Kitanzania na inatajwa kuwa kupitia ziara yake ya ‘Reputation Tour’ ambayo ilimuingizia kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 600

Mwimbaji Beyonce anashika nafasi ya pili ambapo mwimbaji Shakira naakamilisha list hiyo iliyotolewa na Forbes huku mwaka jana orodha hii iliongozwa na mwimbaji Katy Perry ambaye alitajwa kuingiza kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 100 za Kitanzania sawa na dola Mil. 83 za KImarekani.

HII NDIO LIST KAMILI YA WASANII WA KIKE 

1. Taylor Swift – $185M
2. Beyonce – $81M
3. Rihanna – $62M
4. Katy Perry – $57.5M
5. Pink – $57M

6. Ariana Grande – $48M
7. Jennifer Lopez – $43M
8. Lady Gaga – $39.5M
9. Celine Dion – $37.5M
10. Shakira – $35M

VIDEO: MWANZO MWISHO ALIVYOPATIKANA MISS TANZANIA 2019

Soma na hizi

Tupia Comments