Habari za Mastaa

Chris Brown na Drake kuileta video ya ngoma yao ‘Guidance’ (+Picha)

on

Ni headlines za mastaa wawili kutokea nchini Marekani Drake na Chris Brown kuonekana pamoja mitaa ya Miami wakifanya maandalizi ya video ya wimbo wao mpya ‘No Guidance’ ambao pia unapatikana katika Album ya tisa ya Chris ‘Indigo’ ambayo aliiachia June 28,2019

Chris Brown aliwahi  kuongea kuhusu kolabo hiyo na Drake usiku wa sherehe ya birthday yake May 5,2019 na wengi hawakuamini ujio wa ngoma hiyo kutokana na kuhisi kuwa ni kiki pengine inafanyika, mwaka huu 2019 mastaa hao wako tayari kufanya kazi kwa pamoja na kuwathibitishia mashabiki kuwa wamemaliza tofauti zao.

Chris Brown pamoja na Drake walimaliza bifu lao usiku wa October 12,2018 katika tour ya Aubrey & the Three Amigos  baada ya Drake kumpandisha Chris Brown kwenye stage moja na Drake aliwahi kufunguka na kusema kuwa mara ya mwisho kuwa kwenye stage moja na Chris Brown ilikuwa 2009 katika chuo cha Virginia Commonwealth .

PART TWO: HIKI NDICHO KISIWA CHA MSILA WANAFUNZI HUTUMIA MITUMBWI KUVUKA ZIWA KWENDA SHULE

Soma na hizi

Tupia Comments