Habari za Mastaa

Nicki Minaj na mpenzi wake mbioni kufunga ndoa?

on

Kwa mujibu wa mtandao TMZ umeripoti kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo ndoa kati ya rapper Nicki Minaj na mpenzi wake wa sasa Kenneth Petty baada ya kuripotiwa kuwa wawili hao wamefanikiwa kupata leseni ya ndoa jijini Los Angeles.

Watu wa karibu waliuelezea mtandao wa TMZ kuwa wawili hao walisafiri na kuelekea Beverly Hills na walionekana pamoja Mahakamani siku ya Jumatatu ya July 29,2019 wakichukua leseni ya ndoa yao ambayo ilijumuisha makaratasi ya kujaza na Kenneth Petty alionekana kwenye foleni ya watu wanaolipia leseni ya ndoa iliyoandikwa ‘leseni ya ndoa na programu za sherehe tu’

Hata hivyo imeripotiwa kuwa mapema mwezi wa sita kupitia radio ya Nicki Minaj ‘Queen Radio’ alidokeza kuhusu ndoa yake na Kenneth ambaye waliingia kwenye mahusiano mwaka jana 2018 na kuelezwa kuwa walikutana kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 17 hivyo hii itakua ndoa ya kwanza kwa Nicki Minaj.

ULIPITWA NA MANENO YA WHOZU KUHUSU TUNDA? “WATARAJIE NDOA, NISHAMTAMBULISHA KWA WAZAZI”

Soma na hizi

Tupia Comments