Michezo

Ushindi wa Yanga vs Ndanda FC March 31 2016 umeiingiza kwenye nusu fainali

on

March 31 klabu ya Dar Es Salaam Young Africans inayojiandaa na mchezo wake wa klabu Bingwa barani Afrika dhidi ya klabu ya Al Ahly ya Misri, ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa robo fainali ya Kombe la FA.

Yanga ambayo ipo kambini kwa muda mrefu kujiandaa na mchezo wa klabu bingwa, ilifanikiwa kuiadhibu Ndanda FC katika mchezo wake wa robo fainali ya Kombe la FA, Yanga ilianza kufungwa goli na Atupele Green, lakini lilikataliwa na muamuzi wa mechi.

Baada ya Ndanda FC kuonyesha jitihada za kutaka kupata goli Yanga walilazimika kuongeza nguvu ya ziada na Paul Nonga dakika ya 26 akafunga goli la Yanga kuongoza, Ndanda FC walifanya jitihada na dakika ya 57 nahodha wao Kigi Makasy akapachika goli la kusawazisha.

Uzoefu uliwafanya Yanga wafanikiwe kupata goli la pili na ushindi, kwani Ndanda FC walifanya faulo katika eneo la hatari, na muamuzi wa mechi Jimmy Fanuel kutoka Shinyanga akaamua ipigwe penati, Kelvin Yondani kazidi kudhihirisha umahiri wake katika upigaji wa penati kwa kuipachikia Yanga goli la ushindi na kuipeleka nusu fainali.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments