Michezo

Nado wa Azam FC nje miezi 9

on

Kiungo wa Azam FC Iddi Suleiman Nado atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi tisa baada ya kukatika mtulinga wa kati wa goti la kulia (anterior cruciate ligament).

Nado ambaye kwa sasa yuko Cape Town Afrika Kusini katika hospitali ya Vincent Pallotti kwa ajili ya kupatiwa matibabu, akiwa kaambatana na daktari wa Azam FC Mwanandi Mwankemwa.

Nado alipata jeraha hilo November 30 2021 katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar walioshinda 1-0.

Soma na hizi

Tupia Comments