Habari za Mastaa

Mwigizaji Liam aweka wazi kuhusu kuachana na Miley Cyrus

on

Baada ya siku kadhaa kusambaa kwa taarifa kuwa ndoa kati ya mwimbaji Miley Cyrus na mwigizaji Liam Hemsworth imevunjika huku ndoa yao ikiwa imedumu kwa mwaka mmoja na sababu ya kuvunjika kwa  ndoa yao ikiwa haikuwekwa wazi na kubaki kama kitendawili kwa mashabiki.

Mwigizaji Liam alienda mbali na kuutumia ukurasa wake wa instagram kuweka wazi kuwa penzi kati yake na Miley Cyrus limevunjika na kusema kuwa anamtakia afya njema na furaha kwa maisha yake ya mbeleni hata hivyo aliandika kuwa ishu hiyo ni ya kibinafsi na hatokuja kuongea chochote kwa vrombi vya habari na lolote lisemwalo juu yake ni uongo.

“Habari zenu wote, kitu cha harakaharaka nachoweza kusema ni kuwa mimi pamoja na Miley Cyrus tumeachana hivi karibuni namtakia afya njema na furaha huko mbeleni, hiki ni kitu binafsi, sijafanya na sitofanya mazungumzo yoyote na wanahabari au kituo chuchote cha habari. Chochote kitakachozungumzwa kuhusu mimi ni uongo” 

Inaelezwa kuwa Miley Cyrus na Liam walikutana mwaka 2009 na walivalishana pete mwaka 2012 na baadae wawili hao waliachana na kurudiana tena mwaka 20016 na kuamua kufunga ndoa December,2018, hata hivyo Miley Cyrus aliwahi kusikika kwenye mahojiano ya Elle magazine akisema kuwa hapendi kuitwa ‘Mke’ na hawezi kuwa mwaminifu katika ndoa.

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA PRODUCER DUPA NA K LOH WAFUNGUKA KUHUSU FOBY KUWAKWAMISHA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA.

Soma na hizi

Tupia Comments