Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Rapper Nas na ujio wa Album ya ‘The Lost Tape 3&4’

on

Ikiwa ni siku kumi na tano zimepita tokea Rapper Nas atudokeze muendelezo wa album yake ya ‘The Lost Tape 2’ ambayo inatarajia kuachiwa rasmi July 19,2019, sasa rapper huyo ametudokeza tena na ujio wa muendelezo wa Album ya ‘The Lost Tape 3 & 4″.

Inaripotiwa kuwa wakati wa sherehe ndogo iliyoandaliwa na mkali huyo kwa ajili ya kusikiliza ngoma zilizopo ndani ya Album ya ‘Lost Tape 2’, Nas aliamua kufunguka mbele ya marafiki zake na kuweka wazi kuwa tayari ana ngoma za kutosha tu kwa ajili ya Album ya The Lost Tape 3 & 4 na kusema kuwa alirekodi ngoma nyingi kwa kipindi kirefu mpaka sasa.

Album ya ‘The Lost Tape 2’ ni muendelezo wa toleo la kwanza ambalo aliiachia mwaka 2002 album hiyo imeandaliwa na Pharrell, Swizz Beatz, RZA, No I.D., Hit-Boy, Pete Rock, na Kanye West.

“Nimefurahi kuwaona watu wote mmekuja kusikiliza nyimbo tukimaliza hili tutafanya lingine, tokea miaka 17 iliyopita nimefanya ngoma nyingi na nimenandaa ngoma kwaajili ya  Album ya ‘The Lost Tape 3&4”  >>>alisema Nas 

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA MASTAA WAKIWA KWENYE SURA YA KIZEE? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA 

Soma na hizi

Tupia Comments