Premier Bet SwahiliFlix Ad Tigo Ad

Habari za Mastaa

Kesi ya R Kelly kumuambukiza ugonjwa wa zinaa mwanamke yafufuliwa

on

Inaripotiwa kuwa ikiwa bado mwimbaji mkongwe wa RnB R. Kelly akisubiri kupandishwa kizimbani kwa ajili ya kusikiliza mashtaka 11 juu ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mabinti wadogo sasa leo inaripotiwa kuwa mkongwe huyo ameongezewa shtaka lingine.

Inaelezwa kuwa mwaka 2018 mwanamke aliyejulikana kwa jina la Faith Rodgers alifungua mashtaka juu ya R Kelly akidai kuwa aliwahi kuambukizwa ugonjwa wa zinaa (Herpes) na mkongwe huyo bila yeye kufahamu hata hivyo Mamlaka mjini New York walithibitisha taarifa hizo.

Hata hivyo Mwanasheria Elizabeth Geddes amekiri kupata rekodi za matibabu ya R Kelly kutoka kituo cha Afya cha Walgreens zikiwa na uthibitisho kuwa mwimbaji huyo aliwahi kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa zinaa kwenye kituo hicho.

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA MSANII WA NIGERIA KATUA DAR KAMTAJA ELIZABETH MICHAEL, BONYEZA  PLAY HAPA CHINI 

Soma na hizi

Tupia Comments