Habari za Mastaa

Mamlaka Los Angeles kusimamisha ujenzi wa Kanye West (+picha)

on

Baada ya rapper Kanye West kuanzisha mradi wa ujenzi wa nyumba ambazo lengo ni kupunguza mfumo wa makundi uliopo Marekani yani matajiri na maskini sasa inaripotiwa kuwa huenda mradi huo ukasimamishwa na mamlaka ya mjini Los Angeles.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti wakaguzi wametembelea mradi huo kutokana na madai mbalimbali yaliyotolewa na majirani wa eneo hilo ambapo wamelalamika kuwa unaharibu mpangilio wa nyumba za mtaa huo huku meneja mkuu anayesimamia mradi huo alieleza kuwa nyumba hizo ni za muda mfupi na sio za kudumu hivyo hazileti madhara yoyote kwenye mpangilio. 

Hata hivyo imeripotiwa kuwa hakuna ukweli juu ya taarifa za ujenzi huo kuwa ni za muda mfupi na kwa sasa wamepatiwa siku 45 kukabidhi vibali vya ujenzi pamoja na mpango wa ujenzi nje na hapo watalazimika kusisitisha muendelezo wa mradi huo.

Imeripotiwa kuwa nyumba hizo anazomiliki Kanye West zipo ndani ya hekari 30 za ardhi ambayo anaimiliki mjini Calabasas.

VIDEO: MBASHA KAMUOA MUNALOVE? “ANANIKUBALI, MIMI PIA  NAMKUBALI “

Soma na hizi

Tupia Comments