Habari za Mastaa

“Nahitaji kijana wa Arusha anaevutia kama Usher Raymond” Lady Jaydee

on

Lady Jaydee anahitaji kijana mwenye muonekano kama wa msanii wa RnB kutoka nchini Marekani Usher Raymond ili awepo kwenye video ya wimbo wake mpya.

Jaydee ameeleza kuvutiwa na mwanaume mwenye muonekano kama wa Usher Raymond pia ndio aina ya wanaume ambao anawapenda.

“Nakuja Arusha jamani, nikifika huko na-shoot video kabisa lakini nahitaji msaada wenu, nahitaji kijana anaevutia kama Usher ndio awepo kwenye video yangu maana wanaume wa hivyo ndio ‘type’ napenda, kwa hiyo hebu tisheni tuone watu wa Arusha” Lady Jaydee kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Soma na hizi

Tupia Comments