Habari za Mastaa

Nahreel mpaka Nigeria?!! hata Yemi Alade mikononi mwake??

on

.

.

Nahreel, member wa kundi la Navy Kenzo ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka 2015 kwenye tuzo za KILI, mikono yake kuzisuka vizuri hit single kama Nana ya Diamond Platnumz na Nusu Nusu ya Joh Makini kumemfungulia njia na sasa anaona kuna vitu vingine vinakuja.

Akizungumza na millardayo.com alisema..’Kwanza nawashukuru watu kwa kunipigia kura na kuniwezesha mimi kuwa producer bora wa mwaka, na kwa upande wa kazi zipo nyingine zinakuja kuna kazi ya Joh Makini na rapper kutokea Afrika Kusini AKA, Vanessa Mdee nyingine ya Ben Pol kwa hiyo kuna kazi nyingine zinakuja kutoka nje ya Tanzania

Tangu nilipotengeneza wimbo wa Nana ya Diamond na Nusu Nusu ya Joh Makini nimeanza kupokea connection mbalimbali kutoka Nigeria na sehemu mbalimbali kwa mfano Vanessa Mdee pia ametoka kuniambia kuwa Yemi Alade kuwa anataka kufanya kazi na mimi chini ya The Industry Studio kwa hiyo mashabiki wa Nahreel wakae tayari kwa muziki mzuri…”alisema.

Msikilize hapa

  Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments