Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Meek Mill aungana na Jay Z kuanzisha label yake ya muziki (+Video)

on

Rapper Meek Mill ameamua kushirikiana na rapper Jay Z kuanzisha Label yake ya muziki itakayojulikana kama Dream Chaser Records ambayo itakua chini ya kampuni ya Roc Nation , tayari wawili hao wameingia kwenye makubaliano katika makao makuu ya Roc Nation.

Kutokana na makubaliano hayo waliyoyafanya July 24,2019 imeelezwa kuwa Meek Mill atasimama kama kiongozi mkuu wa label hiyo na atahusika kwenye utengenezaji wa mifumo tofauti tofauti kwa wafanyakazi wake pamoja na kuwasaini wasanii ili kuwaendeleza, label hiyo ya Dream Chasers itasimamia shughuli zake yenyewe ikiwemo mikakati ya ubunifu, masoko na mahusiano ya kibiashara.

Jay Z ambaye amekua kwenye kampuni ya Roc Nation kwa muda mrefu sasa amesema kuwa anaamini kuwa Meek Mill atafanya vizuri kutokana na tayari ameshaelewa mfumo mzima wa muziki na anaamini kuwa ataongoza vizuri wasanii wanaokuja na anaona picha kubwa mbele yake.

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA MREMBO ANAEPIGA VITA KUJICHUBUA “UNAWEZA PATA KANSA HATA YA KIZAZI”? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO 

Soma na hizi

Tupia Comments