Habari za Mastaa

Fabolous aibuka na kukanusha taarifa za kuachana na baby mama wake

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapper kutokea Marekani Fabolous ameachana na mke wake Emily B ambapo haikuwekwa wazi taarifa kamili kuhusu kuachana kwa wawili hao na kudaiwa kuwa Fabolous ameanzisha mahusiano na mwanamke mwingine.

Mtandao huo ulizidi kuripoti kuwa Fabolous ameonekana na mwanamke huyo mpya mitaa ya New Jersey wakila bata hata hivyo baada ya saa chache rapper huyo aliibuka na kukanusha taarifa zinazosambaa kuhusu kuachana na Emily B na alisema kuwa tovuti hiyo imemchafua na atachukua hatua kutokana na kuchapisha habari za uongo.

Iliwahi kuripotiwa kuwa mwanzoni mwa mwaka 2018 penzi kati ya Fabolous na Emily B lilianza kuyumba hii ni baada ya Fab kumpiga na kusababisha majeraha makubwa  kwa baby mama wake na pia kumtishia miasma baba yake mzazi.
“Sijawahi kusema nimeachana na Emily, naipenda familia yangu na sisi ni wapenzi ambao tunatengeneza mahusiano yetu, hiyo story ya TMZ ni uongo” >>>aliandika Fabolous kupitia ukurasa wake wa instagram.
“TMZ  wamepost kuhusu lunch mimi kukutana na mwanamke na nikasema kuwa nilikua kwenye date na wakaongeza story ya ujinga kwamba nimeachana na Emily B, hii ni kunichafua naenda kuongea na wanasheria wachukue hatua , hiki kitu kimenisumbua pamoja na familia yangu”

VIDEO: MREMBO ANAEPIGA VITA KUJICHUBUA “UNAWEZA PATA KANSA HATA YA KIZAZI”

Soma na hizi

Tupia Comments