Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

R. Kelly awekwa jela peke yake

on

Ni headlines za mkongwe wa miondoka ya RnB R Kelly ambaye anaripotiwa kupelekwa jela ya peke yake bila kuchanganywa na wafungwa wengine na hivyo kwa upande wake R Kelly ameonekana kufurahishwa na maamuzi hayo yaliyofanywa na Mahakama.

Taarifa hizo zimethibitishwa na mwanasheria anayesimamia kesi hiyo Nicole Blank Becker ambaye kwa upande wake amekiri kuwa ni maamuzi mazuri kwa sababu ameepuka jambo lolote ambalo lingeweza kumtokea kama angechanganywa na wafungwa wengine, imeripotiwa kuwa Jumanne ya July 16,2019  R Kelly alinyimwa dhamana baada ya kukana mashtaka yote yanayomuandama ya kuwanyanyasa kingono mabinti wadogo.

Mwezi May R Kelly alikamatwa tena na kushtakiwa kwa tuhuma za kuhusika na makosa 11 ya unyanyasaji wa kingono ambapo kati ya makosa hayo yalikuwemo yanayohusisha kifungo cha hadi miaka 30 jela.

VIDEO: JACQULINE ‘SITASAHAU MANENO WAZIRI MKUU ALIMWAMBIA MENGI”

Soma na hizi

Tupia Comments