Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Mtaa wapewa jina la Eric Omondi, ‘Eric Omondi Road”

on

Mchekeshaji kutokea Kenya Eric Omondi amekabidhiwa rasmi Mtaa wenye jina lake maeneo ya Kisumu na ame-share taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa instagram, Eric amepewa heshima hii kutokana na kuthaminiwa na mchango anaoutoa kwenye jamii kupitia tasnia ya uchekeshaji.

Eric Omondi amepata umaarufu mkubwa Afrika ya Masahariki na Nchi nyingine kutokana na aina ya uchekeshaji wake aliwahi pia kushinda tuzo ya Mchekeshaji bora Afrika mwaka 2018 kwenye tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA), hata hivyo Eric Omondi amewahasa vijana kutokata tamaa na kufanya kila kitu kwa juhudi.

“Asanteni sana Serikali ya Kisumu kwa hii thamani mliyonipa daima nitafurahia , ninatoa ahadi kuwa mtazidi kujivunia, nitahakikisha nainua jina la Kisumu na la nchi yangu ya Kenya juu na zaidi ya juu, hapa ni nyumbani, mji wangu, Nchi yangu, naomba hii iwe ni motisha kwa kila mtu kwenye Nchi hii, haijalishi we ni nani, unatokea wapi kwa kuamini na kufanya kazi kwa bidii unaweza kuvuna chochote”  >>>aliandika Eric Omondi  

VIDEO: UWOYA KAFUNGUKA “NIKO NA MPENZI, NAKULA BATA, NINA NYUMBA MBEZI BEACH”

Soma na hizi

Tupia Comments