Habari za Mastaa

Show zavunja penzi la Mwimbaji The Weeknd na Bella Hadid

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa penzi kati ya mwanamtindo Bella Hadid na mwimbaji The Weeknd limebaki stori huku sababu kubwa ya kuachana kwao imetajwa kuwa ni muda ambapo wawili hao kubanwa na ratiba za kazi zao.

Imeripotiwa kuwa wawili hao walikutana mwaka 2015 kwenye tamasha la Coachella na October, 2018 penzi kati yao lilionekana kushamiri na baadae kuelezwa kuwa The Weeknd alinunua nyumba ya kifahari mjini New York na kumuomba mpenzi wake huyo kuishi pamoja. Lakini mwaka huu imedaiwa kuwa wawili hao wamekuwa mbali mbali.

Kwa upande wa The Weeknd imeripotiwa kuwa amekuwa busy na kutayarisha album yake mpya ambayo inadaiwa kuachiwa hivi karibuni  na hivyo muda mwingi wamekuwa wakiutumia katika kazi na kushau ishu nzima ya mampenzi.

VIDEO: MAK JUICE KUWAKUTANISHA JUX, VANESSA, SHILOLE NA MASTAA WENGINE KUWASAIDIA WAMAMA

Soma na hizi

Tupia Comments