Michezo

Naibu Spika awapongeza Simba, Wabunge tuisapoti Club Bingwa

on

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson ametoa pongezi kwa team ya Simba SC mara baada ya kufuzu hatua ya robo fainal ya mabingwa wa Afrika ambapo amewataka Wabunge wote nchini bila kujali ushabiki wao kuungana kwa pamoja katika kuwaunga mkono wachezaji pamoja na team nzima.

“Waheshimiwa Wabunge nichukue fursa hii kuwapongeza SIMBA SC kwa kufuzu kuingia robo fainal klabu bingwa Afrika, kuna Wabunge wanaweza wakawa hawajaelewa uzito wa jambo hili lakini kimsingi kama taifa wote tunapaswa tuungane kuwatia moyo wachezaji wetu na club yetu ili iendelee kufanya vizuri kwasababu inapata fursa ya kuitangaza nchi yetu vizuri”

“Kwa hiyo ni muhimu sana hili tukawa tumelielewa ili tuende nalo pamoja kama taifa na ninaamini mashabiki wenzangu wa Yanga wataungana nami katika kuipongeza Simba kwenye hili”-Naibu Spika Dr. Tulia Ackson

Soma na hizi

Tupia Comments