Januari 10, 2022 Dkt. Tulia Ackson ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya USPIKA wa Bunge, Dkt. Tulia amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu msaidizi Mkuu Idara ya Organaizesheni Bw. Solomon Itunda katika Ofisi za Makao makuu ya CCM Dodoma.