Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja amezitaka mamlaka na taasisi zilizochini ya wizara hiyo kuacha mara moja kukamata na kutoa adhabu kwa wananchi wanaovamia mapori na hifadhi badala yake watoe elimu kwani wananchi wengi hawajui umuhimu ya uhufadhi.
Masanja ametoa maelekezo hayo wakati akitatua mgogoro uliodumu kwa mrefu kati ya wananchi na hifadhi unaohusishwa na wananchi 17 wa kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu waliohukumiwa kwa kukiuka na kuingilia maeneo ya uhifadhi.
“Migogoro inajitokeza sisi tunachukua sheria mkononi wakati huohuo mgogoro haujaisha tuwafanye w=Wananchi wawe waelewa ili watusaidie kuyatunza maeneo hatupaswi sisi kung’ang’ania ripoti ya migogoro imekaa halafu wananchi wanaendelea kusurubiwa halafu hawaelewi hata mimi ukiniambia natakiwa niishie hapa kwanini niende nikachokoze nyuki kule lakini kama hawaelewi utawakuta tu huko ndani” Mary Masanja NAIBU WAZIRI WA ALIASILI NA UTALII
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani ameeleza masikitiko yake baada ya wananchi wa Ushetu wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga kukamatwa na kuhukumiwa katika wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora.