Ad

Top Stories

Naibu Waziri Elimu atinga UDSM, atoa maelekezo namna ya kujikinga Covid-19

on

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amevitaka Vyuo vya Elimu ya Juu na vya Kati nchini vinavyoanza masomo Juni 1, 2020 kutoa maelekezo kwa wanafunzi ya jinsi ya Kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya CORONA bila kuwatia hofu. Naibu Waziri Ole Nasha ametoa maelekezo hayo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kukagua namna Chuo Kikuu cha DSM kilivyoandaa mazingira kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya CORONA kwa wanafunzi kuelekea kuanza masomo Juni 1, 2020.

Ole Nasha amesema virusi vya CORONA pamoja na kuwa vimepungua ni vizuri wanafunzi wakachukua tahadhari ya kuendelea kujikinga kwa kuwa haujaisha kabisa ikiwa ni pamoja na vyuo kufuata mwongozo wa serikali juu ya kuwakinga na kutoa elimu ya kujikinga kwa wanafunzi mara kwa mara ili kuhakikisha wanakuwa na afya njema wanapoendelea na masomo yao.

” Napenda kuvisisitiza Vyuo vyote vya Elimu ya Juu na Kati kuendelea kuwalinda wanafunzi kwa kufuata mwongozo uliotolewa na serikali pamoja na kuwapa wanafunzi elimu ya kujikinga bila ya kuwapa hofu,” amesisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.

Naibu Waziri Ole Nasha ametumia fursa hiyo kuwatakia kila lakheri katika masomo wanafunzi wote wanaorudi Vyuoni na Shule na kuwataka kuwa na amani kwani Vyuo na Shule vimejipanga vema huku akiwataka wanafunzi hao kuzingatia miongozi ya kujikinga na kuwakinga wengine na maambukizi ya Virusi vya CORONA Aidha, Naibu Waziri Ole Nasha amevitaka Vyuo vyote vya Elimu ya Juu na Kati kuandaa crash programu ya kutoa mafunzo kwa ajili ya kufidia muda wa masomo ili kuwawezesha kumaliza programu zilizopangwa kufanyika mwaka huu wa masomo

Soma na hizi

Tupia Comments