Naibu Waziri wa ardhi na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amekutana na maafisa ardhi kwa ajili ya kuwakumbusha na kuwahimiza wajibu wao.
“Baada ya ufungaji wa Mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi yaliyofanyika Chuo Cha Mkwawa, Iringa nilipata nafasi kuzungumza na Maafisa Ardhi wa Mkoa wa Iringa na Manispaa ya Iringa”
”Lengo ni kujadili hali ya Kazi na kukumbushana Wajibu wa kila mmoja katika Utendaji”