Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko amewaagiza Watendaji Wakuu wa Nishati akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Maharage Chande kutohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Nishati unaoendelea Jijini Dar es salaam leo na badala yake waende kutatua tatizo la upatikanaji wa umeme ambao kwa sasa unasumbua Wananchi.
Akiongea mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Biteko amesema Wananchi wanachotaka kwa sasa ni upatikanaji wa umeme wa uhakika na kumaliza mgao ambao unaendelea hivyo amewataka waende kusimamia kuhakikisha umeme unarudi katika hali nzuri kama zamani.