Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. Geofrey Pinda, amewataka Madiwani kutumia nafasi zao kukutana na wananchi kuwaelimisha juu ya matumizi ya ardhi ili kuepusha migogoro ambayo imekuwa ikitokea mara kwa mara.
Amesema hayo leo machi 23, 2023 wakati akizungumza katika mkutano wa wadau kujadili utekelezaji mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi uliofanyika kwenye viwanja vya chuo cha maendelo ya wananchi wilayani Kilwa Mkoani Lindi.
Naibu waziri Pinda ameeleza kuwa wananchi wanawakilishwa na viongozi wao waliowachagua katika nafasi mbalimbali kuanzia katika ngazi ya vijiji, hivyo kunapotokea jambo linalohitaji elimu basi Ni vyema viongozi waliopo kuhakikisha kuwa wanatoa elimu ya mambo ya ardhi.
Akizungumzia juu ya urasimishaji wa ardhi, Naibu Waziri amewaahidi wananchi kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa sera na sheria za ardhi Nchini zinafuatwa na kusimamiwa vizuri, ndio maana imekuja na mpango wa kuhakikisha kuwa ardhi ya vijiji inapimwa.
“Wilaya ya Kilwa ni moja ya wilaya ambazo zina ongezeko kubwa la watu ambalo limeenda sambamba na ukuaji wa vijiji hivyo serikali kupitia Rais Dkt.Samia ameandaa mpango madhubuti kuendeleza ardhi nchini”
“Nimesikia maoni ya wananchi na viongozi mbalimbali wakiwepo wabunge wenu, madiwani na watendaji mbalimbalimbali wakiongea kuhusu migogoro ya ardhi, hivyo wizara tukaiingiza kilwa kwenye mpango na vijiji 69 vitahusika kwenye mradi huu katika utaratibu huu wa awali” ameeza Nibu Waziri Pinda
Naibu waziri pia amewataka watendaji wa Wizara ya Ardhi kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya, kufanya kazi za upimaji na umilikishaji wa ardhi kwa kuzingatia haki kwa wananchi wote bila kuangangalia hadhii au nafasi zao katika jamii.
“Msimuhudumia mtu kwa hadhi yake, wahudumieni watu kulingana na haki zao ili kufanya zoezi hili kuwa la heshima kwa Serikali, Taifa na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hiki ndcho ambaco hata waziri wangu Jery Slaa amekuwa akilisisitiza wakati wote”
Awali akitoa salaam za wanachi kwa Naibu waziri, Mkuu wa wilaya ya kilwa Bw Abdallah Mohamd Nyundo, amesema jamii inakabiliwa na changamoyo ya kutotambua maeneo gani ni ya wakulima, yapi ya wafugaji hali ambayo imekuwa ikichangia sana migogoro ya ardhi na kuleta madhara kwaa wananchi.
“Ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu wa Naibu waziri utachukua maoni yetu na kuwayafanyia kazi kupitia mradi huu ambao ni muhimu sana kwa mustakabali wa ukuaji na ustawi wa wananchi wanaoishi katika mano mbalimbali ya wilaya hii”
“Tunayo changamoyo ya kutotambua maeneo gani ni ya wakulima, yapi ya wafugaji hali ambayo imekuwa ikichangia sana migogoro ya ardhi na ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu wa Naibu waziri utachukua maoni yetu na kuwayafanyia kazi kupitia mradi” ameeleza Mkuu wa Wilaya.
Kwa upande wao daadhi ya wananchi wanaoishi katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, wamepongeza zoezi la urasimishaji wa ardhi unaoendelea Wilayani humo, kupitia mradi wa kubosha usalama wa milki za ardhi unaotekelezwa na Wizaa ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Bi.Asia Mohamed kutoka kijiji cha Nanjilinji A amesema “mradi huu utasaidia utazilinda haki za wananchi waliopo, waliopita na hata wajao, tunampongeza sana Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiruhusu Wizara ya ardhi kutekeleza mradi huu”
“Wilaya ya Kilwa ni moja ya maeneo ambayo yalikuwa na migogoro mingi ya ardhi hasa mipaka ya vijiji lakini kupitia mpango huu, tumeshaanza kuona manufaa kwa sababu tayari wataalam wameshaanza kupata elimu na tumeielewa sana” amesisitiza Mzee Kimbwembwe.
Kwa upande wake Athuman Hassan Kingoropi mkazi wa kijiji chapita Wilayani Kilwa, ameipongeza wizara ya Ardhi kwa utekelezaji wa mradi huo wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi akisema kuwa utasaidia kupanga maeneo ya wananchi kufanyia shughuli zao.
“Kupitia mradi huu sasa wananchi tunapata maeneo ya kilimo, ufugaji, makazi, shule, makaburi na vitu vingine vingi, haya mambo sisi hatukuyazoea lakini sasa yanatekelezeka kwenye maeneo yetu na sisi tunatoa ushirikiano kwa 100%” amesema Kingoropi