Duniani

Hakitupwi kitu hapa !!… zile chupa unaziona takataka, Nigeria wamejengea mpaka nyumba.. (+Pichaz)

on

Maisha yanabadilika kila siku, zamani ilikuwa ukikutana na chupa au makopo ya maji au juice unayaona takataka… sasahivi ni dili na watu wameweka nguvu zao kabisa kukusanya makopo na kuyauza !!

Nigeria wamefanya kitu kingine zaidi mtu wangu, umewahi kuona nyumba za makopo??!! Nigeria wamefanya kitu hicho, wamejenga nyumba kwa makopo ambapo ndani ya makopo hayo kumejazwa mchanga halafu makopo yanapangwa vizuri kabisa mpaka inakuwa nyumba ya kuishi.

House3

Sifa nyingine kubwa za hizi nyumba ni kwamba zina uwezo wa kuzuia risasi na pia zinaweza kuzuia moto.

Naija

Kazi ya ujenzi inaendelea namna hii, hatua kwa hatua!!

House4 House6 House7 House8

Unaweza kuwa na swali kwamba chupa kiasi gani au chupa ngapi zinatosha kukamilisha mjengo??!! Jibu lake ni hili hapa, kama unahitaji nyumba ya vyumba viwili inatakiwa kuwepo na chupa 14,000… Umevutiwa na ujenzi wa aina hii mtu wangu ???

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana naMillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments