Habari za Mastaa

King Kiba kasema “Sasa hayupo kimya kama zamani”

on

Leo June 14,2019 mwimbaji wa Bongo Fleva Alikiba amefanya mahojiano na kipindi cha XXL cha Clouds FM baada ya ngoma yake ya ‘Mbio’ kutajwa kwenye jiwe la Wiki ambapo ngoma hiyo iliachiwa rasmi April 26,2019.

Alikiba ameongelea kuhusiana na ishu ya Mtoto wake wa kiume aliyezaa na Mke wake Amina pamoja na suala zima la muziki na kusema kuwa kwa sasa hayupo kimya kama zamani na hata ikitokea akiwa kimya pengo hilo litazibwa na kundi lake la Kings Music.

“Nashukuru Mungu kwa familia yetu kuongezeka na kupata mtoto, mtoto ni baraka na baraka imeongezeka kwenye familia yetu na imekuja wakati sahihi”

“Kwa sasa sipo kimya kama zamani, na kama nitakuwa kimya basi Kings Music inakuwa inasikika na siwezi sema Kings ndiyo wanafanya niwe kimya hapana maana wao wanamuziki wao na mimi nina muziki wangu”>>>alisema Alikiba

VIDEO: BEN POL KAFUNGUKA SAFARI ZAKE ZA NJE, MJENGO, MAGARI YA KIFAHARI YA KWENYE VIDEO NI YA MPENZI WAKE.?

Soma na hizi

Tupia Comments