Habari za Mastaa

Rick Ross azidi kuchimba bifu kati yake na 50 Cent (+video)

on

Inaonekana kama bifu lililopo kati ya rapper Rick Ross na 50 Cent halina dalili yoyote ya kumalizika hii ni baada ya Rick Ross kukataa kufanya ngoma na 50 Cent na kutaja sababu kuwa rapper huyo sio mkali kama miaka kadhaa iliyopita.

Rick Ross aliyasema hayo kupitia mahojiano aliyoyafanya kwenye kipindi cha Big Boy Neighborhood na kusema kuwa kwa sasa yeye ni mfanyabishara na anaona 50 Cent hana thamani kama zamani pia Rick Ross alizungumzia kuhusu Album yake ya 10 ‘Port of Miami 2’, hata hivyo 50 Cent alipata ujumbe kutoka kwa Rick na alimjibu kupitia mahojiano na Complex na akusema kuwa hana mpango wa kufanya kazi na Rick Ross.

“Kiukweli mimi ni Mfanyabiashara, Kama 50 Cent angekuwa na thamani kama zamani ningefanya lakini kwa sasa hapana.” >>> alisema Rick Ross  

ULIPITWA NA ALICHOKISEMA CHUCHU HANS

Soma na hizi

Tupia Comments