Michezo

Ilibidi ahadi ya kuvua nguo mbele ya camera itimizwe baada ya ushindi wa Timu yake..

on

Kila shabiki huwa na hisia zake pindi timu anayoipenda inapokua ikicheza na mara nyingi tumeshuhudia watu wakitoa hadi mbalimbali endapo timu yake itaibuka na ushindi ama la.

Kuna hii stori  ya mtangazaji wa habari za michezo huko Venezuela imenifikia mtu wangu,,yeye aliwaahidi mashabiki kuwa endapo timu yake ya Venezuela itaibuka na ushindi basi atavua nguo zake mbele ya camera.

Sasa baada ya mchezo kumalizika kati ya Venezuela ambayo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Colombia katika mashindano ya Copa America yanayoendelea, mtangazaji huyo alitimiza ahadi yake ya kuvua nguo mbele ya camera wakati akitangaza.

https://www.youtube.com/watch?v=XjdPKrBNiOQ

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie..

Tupia Comments