Tarehe 21 Machi 1990, nchi ya Namibia ilipata uhuru na kujitenga na Afrika Kusini ambapo mwishoni mwa karne ya 19, wakoloni wa Kijerumani, Uingereza na Ureno walianza kuvutana kwa minajili ya kudhibiti na kupora utajiri na maliasili za Namibia.
Namibia imekuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Madola (Commonwealth).
Mwaka 1878 ilikuwa chini ya Waingereza, mnamo mwaka 1884 Wajerumani waliikalia ardhi hiyo na ikawa inaitwa German South West Africa. Wajerumani walitengeneza miundo mbinu ya reli na kilimo.
Hata hivyo kati ya mwaka 1904 hadi 1908 kulitokea mapigano yaliyosababisha watu wengi kupoteza maisha baina ya Waherero na Wanama.
Utawala wa Wajerumani ilifikia kikomo mwaka 1915 ukipigwa na Afrika Kusini. Hata baada ya Vita Vikuu vya Dunia kuisha taifa hilo likasalia kuwa mikononi mwa League of Nations.
Mnamo mwaka 1966 Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa utawala wake juu ya taifa hilo umeisha ndipo Afrika Kusini ilishikilia eneo hilo kwa Sheria ya de facto.
Kilimo, ufugaji, utalii na uchimbaji wa madini kama Uranium, dhahabu, fedha na metali za base zimekuwa muhimili wa uchumi wa taifa hilo ambalo kwa sasa linaongozwa na Rais Hage Geingob ambaye alishika wadhifa huo kuanzia Machi 21, 2015.
Geingob alipokea mikoba ya Hifikepunye Pohamba.
Namibia ilipata uhuru wake kutoka Afrika Kusini Machi 21,baada ya vita vya Uhuru na
kutokana na mapambano ya harakati ya SWAPO chini ya uongozi wa Sam Nujoma.