Bilionea wa kimarekani Elon Musk ameendelea kuwa gumzo mitandaoni kutokana na namna yake ya kuomba radhi baada ya hii kuwekwa kikaangoni na The New York Times kupitia foramu yao ambapo Musk ameyatukana makampuni yanayojiondoa kutangaza biashara zao na mtandao wake wa X (Twitter) wakimtaka aombe radhi baada ya kuchapisha chapisho kuhusu jamii ya kiyahudi.
Musk amesema kuwa ziara yake kwenda Israeli siku ya Jumatatu wiki hii ambapo alikutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu haikua sehemu ya yeye kuomba radhi kwa Wayahudi lakini amekubali kuwa ujumbe aliyochapisha kuhusu watu weupe na jamii hiyo hakikua kitendo cha busara, Musk amekua akipinga kauli ya kuwa Wayahudi wamechangia kikubwa maendeleo ya nchi za Magharibi.
Kutokana na misimamo yake hiyo huenda mtandao wake wa X zamani Twitter ukapoteza takribani dola za kimarekani $75 Milioni kutokana na baadhi ya makampuni kujiondoa kutangaza nao, Kitendo hicho hakimpi mawazo Bilionea huyo hivyo ametuma ujumbe kwa makampuni yote wanaojiondoa kutangaza na X akitumia matusi mazito ya nguoni “Don’t advertise. If someone is going to try and blackmail me with advertising? Blackmail me with money? Go f— yourself,”