Michezo

Namungo FC yalamba dume kazi kwao, udhamini waendelea kujitokeza

on

Ikiwa ina msimu wao wa kwanza Ligi Kuu Tanzania bara club ya Namungo FC ya Lindi imeendelea kuonesha kuaminiwa na makampuni mbalimbali kwa kuendelea kuwekeza kwa kuidhamini club hiyo, hadi sasa Namungo FC ina wadhamini mbalimbali wakiwemo CRDB na Vodacom.

Leo kampuni ya michezo ya ubashiri ya SportPesa imeingia rasmi mkataba wa kuidhamini club hiyo kama sehemu ya wadhamini wakuu kwa mkataba wa mwaka mmoja, SportPesa imeingia mkataba huo wa mwaka mmoja wenye thamani ya Tsh milioni 120.

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Namungo FC Hassan Zidadu, Mkurugenzi utawala na utekelezaji SportPesa Abbas Tarimba na Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao.

Mkataba wa SportPesa na Namungo FC unaanza kufanya kazi kwa kufuata kalenda za kawaida sio za soka, yaani uaanza January hadi December 2020, mkataba umesainiwa leo mbele ya katibu mkuu wa TFF Wilfred Kidao, mwenyekiti wa Namungo FC Hassan Zidadu na mkurugenzi wa utawala na utekelezaji SportPesa Abbas Tarimba.

Soma na hizi

Tupia Comments