Habari za Mastaa

Good news mtu wangu; wimbo wa ‘Nana’ wagonga nafasi ya juu kwenye countdown ya radio Uingereza!

on

nana

Siku chache zilizopita nilikusogezea good news iliyokuwa inawahusu watu wetu Navy Kenzo ambao wimbo wao wa ‘Game’ waliomshirikisha Vanessa Mdee ulishika #1 kwenye countdown ya radio nchini Nigeria.

Licha ya hivyo wasanii wengi wa Bongo Flava wamekuwa wakiiwakilisha Tanzania vizuri sana, wapo akina Joh Makini, Jux, Alikiba na wengine. Kwa kweli sitoacha kusema wasanii wetu wanajituma na kufanya kazi kwa bidii sana.

nana2

Good news nyingine tena inatoka Uingereza mtu wangu na inaandikwa na mtu wetu Diamond Platnumz amabaye kwenye countdown ya DNA Top 5 kwenye radio ya BBC Radio 1Xtra kipindi kinachoendeshwa na DJ Edu wimbo wa Diamond ‘Nana’ aliomshirikisha Flavor kutoka Nigeria umesikika kwenye nafasi ya #1 wiki hii!

nana3

BBC Radio 1Xtra ilichukua time kupitia page yake ya Twitter kumpongeza Diamond kwa kushika nafasi hiyo wiki hii.

nana

Licha ya hayo video ya ‘Nana’ ya Diamond Platnumz iliachiwa mwezi May tarehe 29 ambayo ni miezi 3 iliyopita lakini ukitembelea page ya Youtube ya msanii huyu muda huu utagundua kuwa kwa miezi hiyo 3 tu video hiyo imepata watazamaji Million 4,064,938  na kwa hilo well done Diamond!

Hii ndio Top 5 ya DNA Top 5 wiki hii kwenye BBC Radio 1Xtra..

  1. Diamond feat. FlavourNana
  2. Patoranking feat. Wande Coal – My Woman, My Everything.
  3. Wizkid feat. Drake &Skepta – Ojuelegba (Rmx)
  4. Khulichana feat. Patoranking – No Lie.
  5. Davido feat. Meek Mill – Fans Mi. 

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments