Michezo

Nani asema amemfundisha Ronaldo kila kitu

on

Winga wa kimataifa wa Ureno Luis Nani ametoa kauli ya utani ambayo imekuwa gumzo mitandaoni kuwa mreno mwenzake Cristiano Ronaldo amejifunza vitu vingi kutoka kwake.

“Cristiano Ronaldo ujuzi wote aliokuwa nao kukimbia na kasi nimemfundisha mimi tukiwa timu za vijana (Sporting Lisbon), (Ronaldo) amejifunza vingi kutoka kwangu anajua”

Nani aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa Major League Soccer na alipoulizwa kutaja mchezaji bora aliyewahi kucheza nao katika 5 alizowahi kucheza ndio akamchagua Ronaldo.

Robaldo na Nani wote wametokea katika club ya Sporting Lisbon ya kwao Ureno katika timu za vijana na baadae wote wakatimkia Man United walikodumu kwa pamoja kwa misimu kadhaa na wakicheza timu ya taifa pamoja.

Soma na hizi

Tupia Comments